Latra yaita wadau wanaotaka saa 24

MAMLAKA ya Udhibiti Usafi ri Ardhini (LATRA), imewaita wadau wenye nia ya kutoa huduma za usafi ri wa abiria kwa saa 24 kupeleka maombi ili yachakatwe na kuona ukubwa wa uhitaji kisha kushirikisha mamlaka nyingine na kutoa uamuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usafiri wa Ardhini wa Latra, Johanes Kahatano alisema wametoa fursa hiyo ili kuona kiwango cha uhitaji na kufanya mchakato wa huduma hiyo.

“Tunaomba wananchi na wadau watupe nafasi tufanye maandalizi ya safari za usiku za saa 24, kwa sasa ratiba zetu za safari zinaanza saa tisa usiku kwa mabasi yanayokwenda safari ndefu za zaidi ya saa 14, wale wanaotaka kutoa huduma kwa saa 24 watuletee maombi tufanye uchambuzi,” alisema Kahatano.

Advertisement

Alisema hivi sasa ratiba zao za safari za mabasi ya abiria zinaanza saa tisa usiku kwa mabasi yanayokwenda safari ndefu, na kwa yale yanayokwenda safari za saa nane hadi 12 hawana vibali vya kusafiri usiku na kuwa sasa wanafanya maandalizi ili wenye nia waweze kusafiri muda wa saa 24.

Aliwaonya wadau wa usafirishaji ambao wanasafirisha abiria usiku bila kuwa na kibali, kuacha mara moja huduma hiyo kwa sababu ni hatari kwa maisha ya abiria na mali zao lakini pia kwa vyombo hivyo vya moto.

“Kuna baadhi ya mabasi, zikiwemo Coaster zinafanya safari za usiku bila kuwa na vibali, hii ni hatari, acheni mara moja tunachukua hatua na tutaendelea kuchukua lakini ni vyema kama unataka kutoa huduma hiyo kwa saa 24, leta maombi tuyafanyie kazi,” alisema Kahatano.

Mapema Mei mwaka huu Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Priscus Joseph akiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Latra, Salum Pazzy alisema hakuna mvutano wa muda wa kuanza safari za mabasi kwenda mikoani.

“Tunafanya kazi kwa kushirikiana, suala la kubadilisha ratiba za mabasi awali muda ulikuwa ni mabasi yote lazima yaanze safari saa 12 asubuhi si zaidi ya hapo, lakini baadaye tuliruhusu ratiba zianze saa 11 asubuhi,” alisema Pazzy.

Pazzy alisema utaratibu huo wa majaribio wa kuanza safari saa 11 alfajiri ulianza Novemba mwaka jana na hadi sasa mabasi 180 yamepewa leseni kuanza safari muda huo na kuwa hivi karibuni wamepokea ushauri kutoka bungeni wa kutaka mabasi hayo yafanye safari saa 24.

Alisema walitangazia wadau wanaotaka kutoa huduma hiyo muda huo kwenda Latra na masharti ni lazima madereva wa mabasi hayo wasajiliwe na mamlaka hiyo ili kufahamu dereva nani yuko na gari gani muda huo.

7 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *