“Lengo letu ni kuimarisha uwezo wa kuajiriwa”

BARAZA la Vyuo Vikuu la Afrika Mashariki (IUCEA) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) linaratibu programu ya mafunzo ya uchambuzi wa data kidigitali kwa vijana na wanafunzi mbalimbali waliomaliza vyuo nchini.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kupata ujuzi wa kidigitali utakaosaidia kuwa wabobevu katika soko la ajira katika maeneo mbalimbali.

Mkuu wa program hiyo kutoka GIZ, David Roos amesema hayo Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi vyeti Kwa Wanafunzi wa vyuovikuu walionufaika na mafunzo hayo.Hafla hiyo imefanyika katika Taasisi ya Telnolojia ya Dar es Salaam (DIT).

SOMA: ‘Sekta binafsi, umma zishirikiane kuhusu elimu’

Amesema program hiyO ya mafunzo ni maalum ili kuwawezesha wahitimu wa vyuo vikuu wasio na ajira na mahitaji ya lazima kupata ujuzi wa uchambuzi wa data, taswira, na ustadi wa kutengeneza simulizi ili kuongeza uwezo wao wa kuajiriwa .

Amesema mafunzo hayo ya siku 10, , wahitimu wamepata elimu ya muhimu ya data ujuzi wa uchambuzi wa data, kuongezeka kwa uwezo wa kuajiriwa, na fursa za kazi kwa washiriki kote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki( EAC)

Amesema washiriki walichaguliwa kutoka kundi la wahitimu wa vyuo vikuu wasio na ajira kutoka katika nchi za Burundi, DR Congo, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, na Uganda.

SOMA:EAC yatenga mamilioni ya fedha kukuza Kiswahili

“Kupitia mfululizo huu wa mafunzo, lengo letu ni kuimarisha uwezo wa kuajiriwa na hata kuwezesha vijana kukubalika katika soko la ajira,” amesema Roos na kuongeza kuwa tayari vijana 84 wamepatiwa mafunzo hayo katika nchi wanachama wa EAC.

Mshiriki wa mafunzo hayo Michael Chongeni ambaye ni mhitimu wa uhandisi kwenye Mafuta na gesi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amesema mafunzo hayo yanawezesha kuwa wachambuzi wazuri wa data na ambayo yanaongeza ujuzi.

Habari Zifananazo

Back to top button