Leseni za biashara kutolewa kwa mfumo mmoja

SERIKALI inatarajia kuunganisha mfumo wa utoaji wa leseni za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Tamisemi), hatua itakayofanya leseni zote za biashara nchini kutolewa kupitia mfumo mmoja.

Mfumo huo utahusisha utoaji wa leseni hizo za biashara kupitia njia ya mtandao, lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na hatimaye kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa sheria Brela inahusika na utoaji wa leseni za Kundi A ambazo ni leseni za biashara za kitaifa na kimataifa, ikiwemo viwanda huku Tamisemi ikihusika na utoaji wa leseni za Kundi B, ambazo ni biashara ambazo hazina sura ya kitaifa na kimataifa.

Akizungumza mjini Musoma leo Jumatatu Juni,26,2023 katika mafunzo ya siku tatu ya maofisa biashara kutoka katika halmashauri za mikoa 10, Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Leseni za Biashara kutoka Brela, Tawi Kilumile amesema kuwa mchakato wa kuunganisha mfumo huo upo katika hatua nzuri.

“Hadi kufika mwaka wa fedha ujao nadhani mfumo utakuwa tayari na leseni zitakuwa zinatolewa kwa njia ya mtandao, lakini mfahamu kuwa sisi Brela tayari tulianza kutoa leseni zinazotuhusu tangu mwaka 2018 kwa njia ya mtandao,”amesema .

Amesema kuwa yapo mafanikio yaliyopatikana baada ya wao kuanza kutoa leseni kwa njia ya mtanda,  ambapo idadi ya leseni zinazotolewa kwa mwaka zimeongezeka kutoka 9,200 mwaka 2018 hadi 14,000 kwa mwaka jana.

“Utoaji wa leseni kwa mfumo mmoja kupitia mtandao una faida nyingi kwa wafanyabiashara na serikali kwa ujumla kwani itasaidia kupatikana kwa takwimu halisi ya biashara zilizopo nchini,pia hii itapunguza gharama kwa wafanyabiadhara pale wanapotaka kukata leseni,” amesema.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Juma Chikoka amewataka maofisa biashara kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi, hali ambayo itasaidia katika kutengeneza mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara nchini.

“Sekta ya biashara ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla na ili iweze kufanya vizuri ni lazima watu wa sekta hiyo mfanyekazi kwa weledi na msiwe kikwazo kwa wafanyabiashra badala yake muwe marafiki mkiwaelekeza nini cha kufanya na mkizingatia hayo mtasaidia katika kufikia lengo la serikali la uchumi wa kati,”amesema.

Kuhusu mfumo wa pamoja wa utoaji leseni, Chikoka amesema kuwa uamuzi huo una manufaa katika suala zima la ukuaji wa biashara na utasaidia kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara.

Baadhi ya wafanyabiashara katika Manispaa ya Musoma wamesema mfumo huo wa utaoji wa leseni kupitia mtandao utakuwa na manufaa kwao na kwamba ni suluhisho la changamoto walizokuwa wakikutana nazo.

“Tunatumia gharama kubwa kukata leseni maana unatakiwa ulipe nauli kwenda manispaa baada ya hapo unatakiwa urudi tena siku nyingine hizo zote ni gharama, sasa tukianza kukata kwenye mtandao itakuwa rahisi kwetu,”amesema Musa Misana.

“Kwenda ofisini kulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo suala la rushwa wapo maofisa wengine ambao sio waamifu walikuwa wanaomba rushwa ili akufanyie kazi yako lakini tutakapoanza kukata wenyewe tutaondokana na shida hizo,” amesema Shamsa Ramadhan.

Maofisa biashara wanaoshiriki katika mafunzo hayo ya siku tatu yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu sheria ya leseni na biashara ya mwaka 1972 ni kutoka katika halmashauri za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tabora, Kigoma, Geita, Shinyanga, Mwanza, Kagera na Mara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ruth Prather
Ruth Prather
3 months ago

I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link… 
Try it, you won’t regret it!….. https://workscloud441.pages.dev/

Last edited 3 months ago by Ruth Prather
Theresa J. Evans
Theresa J. Evans
Reply to  Ruth Prather
3 months ago

Make everyone ( $26,000 __ $38,000 ) A Month Online Making money online more than $20k just by doing simple work With No Prior Experience Or Skills Required. Be Your Own Boss And for more info visit any tab this site Thanks a lot just
.
.
open this link.======> http://www.pay.hiring9.com

Anna
Anna
3 months ago

Make everyone c7 ( $26,000 __ $38,000 ) A Month Online Making money online more than $20k just by doing simple work With No Prior Experience Or Skills Required. Be Your Own Boss And for more info visit any tab this site Thanks a lot just
open this link.======> http://Www.SalaryApp1.com

Last edited 3 months ago by Anna
Anna
Anna
3 months ago

Make everyone ( $26,000 __ $38,000 ) A Month d7 Online Making money online more than $20k just by doing simple work With No Prior Experience Or Skills Required. Be Your Own Boss And for more info visit any tab this site Thanks a lot just
open this link.======> http://Www.SalaryApp1.com

Last edited 3 months ago by Anna
Eva
Eva
3 months ago

I’m making more than $75k by just doing very easy and simple online job from home.Last month my friend sis received $94280 from this work by just giving only 2 to 3 hrs a day.Everybody start earning money online. visit for more details…
 
 See………..>>  https://Www.Easywork7.com

MelanyDorman
MelanyDorman
Reply to  Eva
3 months ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ https://onlinesite76.blogspot.com/

Last edited 3 months ago by MelanyDorman
Back to top button
6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x