LIBERIA : SPIKA wa Baraza la Wawakilishi la Liberia, Jonathan Fonati Koffa, amekanusha kuhusika na moto mkubwa ulioiteketeza jengo la Bunge.
Moto huo ulitokea jumatano, siku moja baada ya mipango ya kumwondoa Koffa madarakani na kuzua maandamano makubwa.
Serikali nchini humo imeanzisha uchunguzi na kutoa zawadi ya dola 5,000 kwa taarifa za wahusika.
“Tunaomba uchunguzi huru wa kimataifa,” alisema Koffa. SOMA: Rais Liberia kuangalia upya sekta ya madini
Mzozo wa madaraka bungeni bado unaendelea, huku baadhi ya wabunge wakitaka kumuondoa Koffa, na wengine kupinga hatua hiyo kama kinyume cha katiba.