PAZIA la Ligi Kuu ya mpira wa miguu kwa wanawake Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 linafunguliwa leo kwa michezo mitano viwanja tofauti.
Bingwa wa simu uliopita Simba Queens itaanza kampeni kutetea taji hilo dhidi ya Mlandizi Queens kwenye uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni Dar es salaam.
Miamba mingine ya soka la wanawake Yanga Princess itaanza kampeni ugenini dhidi ya Bunda Queens kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma mkoa wa Mara.
SOMA: Simba, Yanga waua Ligi Kuu Wanawake
Bingwa wa Ngao ya Jamii kwa wanawake, JKT Queens itakuwa mgeni wa Alliance Girls kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwania pointi za mchezo wa kwanza.
Ilyokuwa Amani Queens ambayo sasa inaitwa Mashujaa Queens itaikaribisha Gets Program iliyopanda daraja kwenye uwanja wa Maj Gen Isamuhyo ulipo Mbweni, Dar es Salaam.
Katika kipute kingine Fountain Gate Princess itaikaribisha Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.