Ligi ya vijana Arumeru kuendelea kesho

ARUSHA: MZUNGUKO wa pili wa ligi ya vijana wenye umri chini ya miaka 11-13 wilayani Arumeru mkoani Arusha unaendelea kesho Machi 21 kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti.

Ligi hiyo inaendelea kuwa chachu ya kukuza vipaji vya vijana huku ikiwapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kufungua milango ya kuchezwa soka la ushindani katika ngazi za juu.

Katika michezo ya vijana walio na umri wa chini ya miaka 11, vinara wa ligi hiyo Young Boys Academy watacheza dhidi ya CTIDO, Satino Academy dhidi ya Future Stars na Kiytec itachuana na Peace Youth Academy.

Msimamo wa ligi ya vijana chini ya miaka 11, Young Boys inaongoza ikiwa imejikusanyia pointi 13 ikifuatiwa na Future Stars pointi 12 nafasi ya tatu Satino Academy pointi 10, CTIDO pointi 6 nafasi ya nne huku nafasi ya tano na Peace Academy pointi 3 na Kiytec inashika nafasi ya sita ikiwa haina pointi.

Kwa umri wa chini ya miaka 13, michezo minne itachezwa ambapo mchezo wa kwanza Young boys itaikaribisha Nshupu Academy, Future Stars dhidi ya Peace, CTIDO dhidi ya Satino na Follow your dream itamaliza ratiba dhidi ya Kiytec, michezo yote ikichezwa katika viwanja vya Future stars vilivyopo Burka,Olasiti.

Timu ya Young Boys kwa mara nyingine inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa imeshinda michezo yote saba ya mzunguko wa kwanza kwa kujikusanyia pointi 21 ikifuatiwa na Follow Your Dream ikiwa na pointi 18 huku Future Stars ikiwa nafasi ya tatu kwa Pointi 13.

Mashindano hayo yanafanyika kwa msimu wa tatu yakiandaliwa na Taasisi ya Young boys yenye makazi yake wilayani Arumeru yakilenga kuangazia soka la vijana,kuibua na kutoa fursa mbalimbali za ndani na nje kwa wachezaji wanaochipukia.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. F8BET – là thương hiệu uy tín nhất hiện nay. Cung cấp các trò chơi đa dạng thể thao, casino … với tỷ lệ trả thưởng cao, nhanh tay đăng ký tặng +68K.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button