Lionel Messi afikisha mabao 846

MSHAMBULIAJI wa Argentina, Lionel Messi amefikisha mabao 846 mara baada ya kufunga matatu katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Bolivia jana.

Katika ushindi huo, Messi ametoa pasi mbili za mabao, hivyo kuhusika kwenye mabao matato. Messi amefunga mabao hayo akiwa na klabu za Barcelona, PSG, Inter Miami na timu ya taifa ya Argentina.

Nyota huyo wa Inter Miami ameweka rekodi ya kufunga hat-trick yake ya 10 akiwa na Argentina.

Advertisement

SOMA: Messi: Sikuwa tayari kuondoka Barcelona

Hat-trick ya kwanza ya Messi kwa La Albiceleste ilikuwa mwaka 2012 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Uswizi. Kwa ujumla, Messi sasa ana mabao 112 akiwa na Argentina.