TETESI za usajili kimataifa zinasema Liverpool imeripotiwa kumfuatilia kwa karibu kiungo wa SC Freiburg inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani-Bundesliga, Merlin Rohl, mwenye umri wa miaka 21, kwa ajili ya uwezekano wa uhamisho.(Caught offside)
Kocha Erik ten Hag ameiomba Manchester United kumfuatilia mshambuliaji wa RB Leipzig Benjamin Sesko ili kujaribu kutatua tatizo la ufungaji linalowakabili ‘mashetani hao wekundu’. (El Nacional – Spain)
SOMA: Tetesi za usajili Ulaya
Mshambuliaji wa Sporting CP Viktor Gyokeres na winga wa Athletic Club, Nico Williams wameibuka kuwa walengwa wawili muhimu wa usajili Liverpool huku hatma ya Mohamed Salah ikiwa bado ni kitendawili.
Pia Anthony Gordon wa Newcastle United na Ollie Watkins wa Aston Villa wapo kwenye rada ya Liverpool.(CaughtOffside)
Barcelona ni miongoni mwa vinara wanaowania kumsajili Jamal Musiala iwapo ataondoka Bayern Munich kwani angependa kuungana tena na kocha wa zamani, Hansi Flick. (El Nacional – Spain)