Lokassa Ya M’Bongo afariki dunia

MKONGWE wa kupiga gitaa la rhythm kutoka nchini DR Congo, Lokassa Kasia Dennis maarufu Ya M’Bongo  au Ya Mbongo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76, baada ya kuugua kwa muda mrefu nchini Marekani.

Lokassa ambaye alikwa kiongozi wa bendi maarufu ya Soukous Stars, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Standard wa nchini Kenya, taarifa ya promota wa muziki wa Congo anayeishi Nairobi, Tabu Osusa, Ya M’Bongo alikuwa akiugua magonjwa yanayohusiana na moyo.

Lokassa atakumbukwa kwa nyimbo nzuri ambazo alishiriki kuziandaa na kupiga gitaa kama Bonne Annee, Monica, Marie-Josse na Assitou.

Habari Zifananazo

Back to top button