Mbunge Wa Viti Maalum anayetokana na Asasi za Kiraia Tanzania Bara, Neema Lugangira amewaongoza wakazi wa mtaa wa Rwome kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba kupiga kura ya kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa.
Akiwa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Sekondari Kahororo amesema amevutuwa na wingi wa watu waliojitokeza kupiga kura na utaratibu wa wananchi kupiga kura unavyofuatwa.
“Nimeshuhudia shauku na wingi wa watu waliokuja kupiga kura hakika wananchi wameamua kama kuna watu hawajatoka nyumbani kuja kupiga kura wafike haraka ili kutimiza wajibu na kupata haki ya kuwapata viongozi wao mazingira ni mazuri na hauchelewi”anasema Lugangira