Maafisa wa madini mbaroni Rwanda

KIGALI: MAAFISA watatu waandamizi wa Bodi ya Migodi, Petroli na Gesi nchini Rwanda na wafanyabiashara wanne wamekamatwa kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya mamlaka.

Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) imesema watuhumiwa hao wanashikiliwa Kigali kwa mahojiano zaidi kuhusu makosa yanayowakabili.

Waliozuiliwa ni Augustin Rwomushana, John Kanyangira na Richard Niyongabo, wakihusishwa na vitendo vya ufisadi, kujilimbikizia mali na utakatishaji wa fedha.

Taarifa za uchunguzi zinasema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Umoja wa Ulaya mwezi Machi kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa bodi hiyo kwa madai ya kuunga mkono waasi wa M23.

Rwanda imetajwa mara kadhaa kuhusika na waasi wa M23 wanaodhibiti maeneo yenye madini mashariki mwa DRC , ingawa serikali ya Kigali imekuwa ikikanusha tuhuma hizo.

SOMA: Mauzo ya nje Rwanda yapanda

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button