Marburg yapungua Rwanda

RWANDA : MAAMBUKIZI ya virusi vya ugonjwa wa  Marburg nchini Rwanda yamepungua baada ya watu waliokuwa  hatarini kuanza kupatiwa chanjo.

Waziri wa afya nchini Rwanda Sabin Nsanzimana amesema tangu serikali kwa kushirikiana na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC  kutoa chanjo maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Hatahivyo,Mkuu wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC Jean Kaseya amesema licha ya kupungua kwa maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Marburg kwa sasa wanakabiliana na tatizo la Mpox ambalo limeshafika katika nchi sita Barani Afrika.

Advertisement

SOMA: Tumeendelea kudhibiti ugonjwa wa virusi vya marburg’