MABADILIKO ya Tabianchi yametajwa kuwa miongoni mwa chanzo cha ongezeko la migogoro kati ya wananchi na wanyama pori kutokana na mwingiliano unaosababishwa na uhitaji mkubwa wa maeneno na maji.
Akizungumza wakati wa semina ya Waandishi wa habari wa Mazingira leo iliyofanyika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, meneja wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika mradi wa ‘USAID Tuhifadhi Maliasili’ kutoka Taasisi ya Kimatifa ya Utafiti (RTI International) Elikana Kalumanga amesema mgogoro huo unatokana na mvua kupungua hali inayopelekea ukame na vyanzo vya maji kukauka.
“Wanayama kama simba wanavamia makazi ya watu lakini pia tembo wanaingia kwenye mashamba kunakuwa na migogoro kwani hakuna malisho hata wananchi wanaingia katika sehemu za maji na maeneno ambayo wanaishi wanayama ,”ameeleza.
Amesema mabadiliko ya tabianchi yanasababisha pia ongezeko la joto hali ambayo inaweza kusababisha wanyama kutafuta mazingira mazuri kwako hivyo watalazimika kautoka sehemu moja hadi nyingine.
“Ukame uliokithiri moja wapo ya madhara ni mazao hayastawi na vyanzo vya maji yanakauka na sehemu zilizosalia na maji wanayapori wanahitaji na wananchi wanakimbilia hapo kwaajili ya kuzalisha mazao na kuepeleka mifugo yao migogoro.
Aidha amefafanua kuwa moja wapo ya namna ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi wanaangalia uwezekano wa kusaidiana na serikali na wadau kuhakikisha shoroba zinahifadhiwa ili wanayama pori wanapopata ukame wanaweza kutembea kwenda sehemu nyingine kupata mahitaji yao kama maji na malisho.
“kwasababu wanyama wanahitaji kupita kutoka eneo moja kwenda lingine na sehemu zingine ni shoroba lakini kama halipo wanakatisha kwenye mashamba ya watu na makazi.
Amesema Waandishi wa habari wanajukumu la kuelimisha wananchi kuhusu mabadiliko ya tabianchi lakini pia juhudi ambazo zinafanyika kupambana kama kuhakikisha misitu inahifadhiwa na kupandwa kwa miti kwa sehehmu ambazo hamna kwasababu moja ya hewa ya ukaa inayochangia katika mabadiliko inasababisha na kabindioxide ambapo miti inasaidia kupunguza.
Kalumanga amesema wanatekeleza mradi katika maeneno saba ambayo ni kipaumbele cha serikali ambayo ilianisha maeneno ya shoroba za wanayamapori 61.