Mabasi sita yarudishiwa leseni

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imerejesha huduma ya leseni ya mabasi sita ya Usafirishaji wa Mabasi ya Kampuni ya Katarama iliyokuwa imewafungia leseni ya usafirishaji kwa kosa la kuchezea mfumo mwendo kwenye mabasi hayo.

Leseni hiyo ya usafirishaji kwenye kampuni hiyo ilisitishwa Septemba 13 mwaka huu.

SOMA: LATRA yatangaza ruti mpya 10 daladala Dar

Mkuu wa Uhusiano na Mawasilano LATRA, Salum Pazzy ametoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam leo kwenye mkutano na waandishi wa habari mbele ya na mmiliki wa kampuni ya Karatama.

“Tumerejesha huduma ya mabasi sita kati ya mabasi kumi yaliyokuwa yamesitishiwa huduma ya leseni hatua hiyo ilifuatia uchunguzi wa awali uliofanyika na kubaini kosa la kuingilia mfumo wa mabasi kwa njia ya kubadili sehemu ya kifaa cha mwenendo wa mabasi kwa kuweka kifaa kingine kilichosababisha utumaji wa taarifa potofu kwa mfumo wa VTS,”

“Katika uchunguzi huo wa awali kosa lilibainika kwenye mabasi mawili namba T.420 EDR na namba T.836 EDR mara baada ya kusitisha huduma mamlaka ilifanya uchunguzi kwenye mabadi yote 10 na kubaini mabasi mengine mawili namba T.835 EDR na namba T.435 DXE kuwa yamefanyiwa aina hiyo hiyo ya kuingilia mfumo wa VTS,” amesema Pazzy.

Mmiliki wa kampuni ya Katarama, Laurian Katarama amesema watafuata taratibu na sheria za barabarani na kuwaomba abiria msamaha kwa kutokana na kusitisha huduma kwa kipindi kutokana na kusitishwa kwa leseni hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button