Machinga, bodaboda Dar wagomea maandamano Chadema

DAR ES SALAAM: SHIRIKISHO la Madereva Bodaboda na Bajaji na Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Nchini (SHIUMA) wamesema hawapo tayari kushiriki maandamano na shughuli zozote zinazihusisha uvunjifu wa amani na kusababisha kukosa utulivu katika utendaji wao wa kazi.

Pia wamesema shughuli zao zinategemea amani na utulivu, hivyo wameomba jeshi la polisi washighulikie hilo ili waweze kufanya shughuli zao kwa amani sehemu zao za kazi zisitumike kwa shughuli za kisiasa.

Hayo yameelezwa leo Aprili 21,2025 Dar es salaam katika mkutano uliofanyika na taasisi hizo za kijamii wakizungumza na waandishi wakieleza wazi nia yao ya kutotumika katika shughuli na maandamano Aprili 24,2025 kama Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche alivyowataka washiriki siku hiyo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Madereva Bodaboda na Bajaji taifa na Mkoa wa Dar es salaam, Said Kagomba amesema kuwa madereva bodaboda na bajaji wasitumike kama ngazi kwani wanajitambua na wanatumia shughuli hizo kusomesha na kuendasha maisha yao hivyo hawatoshiriki maandamano hayo.

Akifafafanua hilo Kagomba amesema kuwa miaka ya nyuma bodaboda walikuwa na changamoto ya kutoruhusiwa kuingia na kufanya shughuli zao mjini na hakutoka kiongozi yoyote kutoka Chadema kusimama na kuwapigania kwa chochote akini serikali imeweza kuwapatia nafasi.

“Madereva wa usafirishaji tulipata tabu sana lakini hatujawahi ona hata siku moja kwamba hicho chama kinatuhitaji leo na kuona umuhimu wetu wa kuweza kushirikiana nao, lakini leo tunafanya kazi mahala popote unaweza kuingia mahala popote na kubeba abiria kuelekea naye popote,” amesema Kagomba.

Ameongeza kuwa Rais Samia alishatoa maridhiano ya kisisasa, hivyo kama wao wanachangamoto za kisisasa wakakutane na rais wakae chini wafanye majadiliano kwasababu wanaamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani,hivyo hawawezi kwenda kuandamana kwa sababu sio sahii kwani kwani wanawatu wanaowategemea.

Kagomba amesema uwa kila mtu anachama chake cha siasa lakini linapokuja sualala uvunjifu wa amani hawapo tayari kuwekw mstari wa mbele na wanataka kufanya shughuli zao kwa amani.

Naye Mwenyekiti wa Waendesha Bajaji wenye ulemavu wa Ferry-Kariakoo, Gosbart Kajaraba, ameeleza kuwa wao wanatanguliza utulivu na maendeleo kwa sababu wanataka mazingira salama ya kufanya kazi kwa sababu maandamano yanahamasisha uvunjifu wa amani na kuvuruga shughuli zao.

Makamu Mwenyekiti wa Wajasiriamali Wadogo nchini, Steven Lusinde amesema anaziomba mamlaka husika ziwasaidia watu maeneo ya kwenda kufanyia mikutano na sio maeneo wamachinga wanayofanyia kazi na biashara zao.

Katika hatua nyingine, viongozi wa machinga kutoka Soko la Ilala wakiongozwa na Bakari Mkupa, wamesema tayari wamewasiliana na masoko mengine kuhakikisha hakuna mfanyabiashara atakayeshiriki maandamano hayo na hawapo tayari kutumia masoko kwa shughuli za kisisasa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button