Harambee yafunguliwa kuisaidia Lebanon

PARIS: RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron leo amefungua mkutano wa harambee kuisadia Lebanon mjini Paris, kuchangisha mamilioni ya dola na kuendeleza juhudi za kidiplomasia  za kutafuta ufumbuzi  wa vita vinavyoikabili nchi hiyo.

Ufaransa, ambayo ina mahusiano ya kihistoria na Lebanon, pia inataka kutumia mkutano huo kutafuta njia ya kuongezwa msaada wa kibinadamu nchini Lebanon.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot ameahidi kwamba Ufaransa haitoitupa mkono Lebanon.

Advertisement

Hatahivyo  Serikali ya Ufaransa imeahidi  kuendeleza  uhusiano wake wa karibu wa kihistoria na Lebanon na kuendelea kuisaidia nchi hiyo hasa katika kipindi hiki cha mapigano .

” Ufaransa tutaendelea kutoa  misaada ya kibinadamu na kuunga mkono jumuiya ya kimataifa na vikosi vya jeshi la Lebanon kwa lengo la kuimarisha usalama, hasa kusini mwa Lebanon.”Alisema Rais Macron.

SOMA : UN, Lebanon waomba ufadhili dola mil 426