UFARANSA: Rais wa Ufaransa,Emmanuel Macron amempigia simu Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian na kumuomba aache kuiunga mkono Urusi katika vita dhidi ya Ukraine.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Ufaransa, imedai kuwa mazungumzo haya ni ya kwanza kati ya marais hawa wawili tangu Masoud Pezeshkian kuingia madarakani.
Macron pia amemuomba Rais Pezekhsan kufanya kila linalowezekana ili kuepusha kuongezeka kwa harakati za kijeshi kati ya Israel na Lebanon kufuatia shambulio la hivi karibuni la roketi kwenye Milima ya Golan ambalo linadaiwa kufanywa na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Tehran.
Macron amesema Urusi ilipoivamia Ukraine, Iran ilishirikiana na Urusi kuishambulia Ukraine jambo ambalo inabidi lisitishwe.
Katika mazungumzo hayo, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amemuhakikishia Rais Macron kwamba anampango wa kurejesha mahusiano na nchi za magharibi.
SOMA: Rais wa Iran afariki dunia
Masoud Pezeshkian anachukuliwa kama mwanasiasa mwenye msimamo wa wastani ukilinganisha na Rais wa Iran aliyepita Ibrahim Raisi aliyefariki hivi karibuni katika ajali ya ndege.