IMEELEZWA uwepo wa kambi za madaktari bingwa wa Rais Samia Suluhu Hassan umesaidia kuimarisha hali ya utoaji huduma za afya nchini sambamba na kuwapunguzia adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya za kibobezi.
Hayo yamesemwa na leo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani wakati wa mapokezi ya madaktari bingwa 77 wa Rais Samia ambao wapo mkoani Tanga kutoa huduma za matibabu ya kibobezi kwenye Halimashauri 11 za mkoa huo .
Amesema kuwa kambi hizo ni dhamira ya dhati ya Rais Samia ya kuona afya za wananchi zinaimarika lakini na kuwapunguzia muda pamoja na gharama ya kufuata huduma za afya maeneo ya mbali.
“Niwaombe kambi hiyo itumike katika kuwajengea ujuzi wataalamu wetu wa afya waliopo kwenye ngazi za Halimashauri lakini mkafungue na wodi za watoto chini ya umri ya miaka mitano ambazo zimejengwa na kuwekewa vifaa lakini bado hazijaamza kutoa huduma,”amesema RC Buriani.
Hata hivyo Ofisa Programu Idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Joachim Masunga amesema kuwa jumla ya madaktari bingwa 77 waweze kuletwa mkoa huo Kwa ajili ya kutoa huduma za kibobezi Kwa wagonjwa kwenye Halimashauri 11 mkoani Tanga.
“Madaktari hawa wataweka kambi ya siku sita kwenye hospitali za halimashauri nane ambapo matarajio ni kuona jumla ya wagonjwa 3000,”amesema Masunga