Madudu haya kero kwa wawekezaji – Mwigulu

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema kuwa wawekezaji wa nje  wamekuwa wakikutana na vikwazo vingi kuliko uwezeshaji ndani ya serikali na hata kwa wananchi.

Akizungumza leo Juni 15,2023 Mwigulu amesema licha ya wawekezaji hao wanaleta mtaji, teknolojia, ajira, kuongeza mapato kwa Serikali na kukuza uchumi, uzoefu unaonesha kuwa, wawekezaji hao wamekuwa wakikumbana na vikwazo mara kwa mara

“Kwa upande wa Serikali, kila ofisi anayoingia mwekezaji, wanatafuta kipengele kinachoweza kumkwamisha ili wazo lake likwame badala ya kutafuta namna nzuri ya kufanikisha uwekezaji.”Amesema Mwigulu na kuongeza

“Kwa upande wa wananchi, atakutana na mtazamo wa uraiani mathalani mwekezaji anapofika na mtaji wa kuwekeza kwenye meli na bandari ya uvuvi wa samaki kwenye kina kirefu ambao hata wasipovuliwa watahama na kuvuliwa sehemu nyingine, mosi utasikia ana fedha kweli, huyu sio tapeli kweli?

Pili wakijiridhisha ana fedha, utasikia huyu hatatuibia kweli?

tatu akitokea anayeshauri kwamba nadhani uwekezaji huu ni muhimu kwa ajili ya nchi utasikia huyu lazima ameshapewa fedha, amelambishwa asali huyu. Ni lazima tukubali uwekezaji ikiwemo kuwapa majina mazuri wanaobeba hatima za wengine,” amesema Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba

Habari Zifananazo

Back to top button