VENEZUELA: Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesisitiza kuwa chama chake kiko tayari kuwasilisha majumuisho yote ya kura kutokana na uchaguzi wenye utata nchini humo baada ya waangalizi wa uchaguzi kusema kuwa ” uchaguzi hauwezi kuchukuliwa kuwa wa kidemokrasia”.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Uchaguzi (CNE) lilithibitisha Nicholas Maduro ameshinda uchaguzi huo.
Hadi sasa kambi ya upinzani nchini humo imedai kuwa hesabu za wapigakura zinaonyesha wazi mgombea wao Edmundo González alishinda kwa kura nyingi.
Ushindi wa Maduro uliwafanya wananchi nchini humo kuandamana kupinga matokeo hayo ya uchaguzi huku mashirika yasiyo ya kiserikali yakitoa taarifa za vifo vya watu 11 huku wengine wakijeruhiwa katika ghasia za maandamano.
SOMA: Nicholas Maduro apita tena urais
Akizungumza na wanahabari nchini humo kuhusu matokeo ya uchaguzi Maduro amesema serikali yake iliamua kutochapisha matokeo ya uchaguzi kutokana na udukuzi uliofanywa kwenye tovuti ya baraza la uchaguzi.