Maendeleo vitendo sio propaganda

SHINYANGA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema maendeleo ya kweli yanahitaji vitendo na si propaganda, kikieleza kudhihirisha hayo kupitia utekelezaji wa yale yote waliyoyaeleza katika Ilani ya uchaguzi 2025/30.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi an Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongozi ameeleza hayo leo Machi 5,2026 alipotembelea mradi wa kufua umeme wa jua (REA) katika kijiji cha Kayenze Kata Ya Ukune Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama, Shinyanga.

Imeelezwa kuwa mradi huo umekamilijswa kwa kipindi cha mwaka mmoja na umegharimu kiasi cha Sh bilioni 11.6 na unachangia megawati tano katika gridi ya taifa, na unahusisha ushirikiano katika ya serikali na mwekezaji ambaye ni kampuni ya kichina.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo Kihongosi amesema CCM kama ilivyoahidi kwenye ilani maendeleo yaliyosemwa yatafika katika kila maeneo haliyokusudiwa akieleza kuwa miaka mitano hadi 10 iliyopita umeme haukuwepo kwenye vijiji lakini leo kila kijiji kina umeme.

“Leo hapa tumepata taarifa kwamba vijiji na vitongoji 136 wakandarasi wapo saiti vimebaki vijiji kama 100 na kidogo ambavyo kabla ya mwaka 2030 anu 2029 serikali za mitaa maana hake vitongoji vyote vitawaka umeme, wasije watu wakawaambia hakuna kilichofanyika,” amesema Kihongosi.

Ameongeza kuwa wananchi yaliyofanyika yapo na yanaonekana, hivyo wasipotoshwe kuambiwa hakuna kilichofanyika akisisitiza katika maendeleo ya kweli hayahitaji propaganda bali vitendo.

“Kwenye kujenga uchumi au maisha au mafanikio hatujitaji maneneo tunahitaji bitendo na ndo kama hivi sola ipo hapaa, zahanati inajengwa itakabidhiw amuda si mrefu, kuanza matumizi ya nishati safi na mengineyo,” amesisitiza Kihongosi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button