Mafuriko yaua 33 Beijing

IDADI ya watu waliofariki kutokana na mafuriko katika mji mkuu wa China, Beijing imeongezeka na kufikia 33 wakiwemo waokoaji watano huku watu wengine 18 wakiwa hawajulikani walipo.

Mafuriko hayo yalianza Agosti 5, 2023 Magharibi mwa Beijing na kusababisha kuporomoka ya nyumba 59,000 na uharibifu wa nyumba 150,000.

Barabara nyingi pia ziliharibiwa, pamoja na madaraja zaidi ya 100, Xia Linmao, Makamu Meya wa Beijing, alisema katika mkutano na waandishi wa habari leo.

“Ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wale waliofariki wakiwa kazini na waathiriwa wengine,” Linmao aliwaambia waandishi wa habari, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la CCTV.

Habari Zifananazo

Back to top button