‘Magari yatumike ukaguzi miradi ya maendeleo’

TANGA; Serikali inatarajiA kutumia kiasi cha Sh Bil 1.1 kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya magari katika Mkoa Tanga, Ili kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani wakati wa hafla ya ugawaji wa magari  ya Wakuu wa Wilaya za Kilindi, Korogwe na Pangani mkoani humo.

Advertisement

Amesema kuwa serikali imekuwa ikiendelea kuboresha mazingira ya kazi Kwa watendaji wake, Ili kuhakikisha wanatoa huduma bora na kwa wakati wa wananchi wake

Soma: Ma-DC Ileje, Mbozi wakabidhiwa magari mapya

“Ni Imani yangi magari haya yatatumia katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo, kufanya ziara za kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwenye maeneo yenu na sio vinginevyo,”amesema RC Buriani.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Kilindi Hashim Mgandilwa, amesema kuwa magari hayo yameongeza ari na nguvu ya kufanya shughuli za kuhudumia wananchi pamoja na usimamizi wa miradi .

“Wilaya ya Kilindi ina maeneo makubwa ya utawala hivyo, kwa usafiri huu umetuongezea ari ya kufanya kazi Kwa bidii hususani za kutatua na kusimamia changamoto za wananchi wetu,”amesema Mgandilwa.