Mahmoud mwenyekiti mpya kamisheni AU

ADDIS ABABA: Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibout, Mahmoud Youssouf amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Kiongozi huyo ameshinda nafasi hiyo kwa kuwashinda Raila Odinga wa Kenya na Richard Randriamandrato aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Madagascar.

Aidha taarifa ya mtandao wa ‘Reuters’ imeeleza Mahamoud ametangazwa mshindi baada raundi kadhaa za uchaguzi kutokana na kipengele cha 2/3 kilichoeleza kuwa mshindi ni lazima apate 2/3 ya kura zote 49 kutoka kwa nchi zilizoshiriki kupiga kura.

Advertisement

Katika raundi ya kwanza Raila odinga alishinda duru hiyo, lakini alishindwa kufikisha 2/3 na hivyo kuendelea na raundi nyngine.

Mshiriki Richard Randriamandrato alienguliwa katika kinyang’anyiro hiko katika raundi ya pili na hivyo uchaguzi kubaki kati ya odinga na Youssef.

Youssouf aliongoza katika raundi ya 3, 4, 5 ila bado hakufika 2/3 ya kura, ambapo katika raundi ya tano Youssouf alipata kura 25 dhidi ya 21 za Odinga.

Youssef alishinda pia raundi ya sita kwa kupata kura 26 dhidi ya 22, na hivyo Odinga kulazimika kujitoa na kuacha Youssouf apigiwe kura, ambapo alifanikiwa kufikisha 2/3 na kutangazwa kua mshindi na mwenyekiti mpya wa AUC.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *