Majaliwa aagiza mwenye jengo atafutwe

DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta mhusika wa jengo lililoanguka Novemba 15, na kusababisha vifo vya watu 16, na wengine kuokolewa kwenye vifusi.

Akizungumza leo Novemba 18, katika tukio la kuiaga miili ya watu 16, viwanja wa Mnazi Mmoja Kariakoo, Dar es Salaam, Majaliwa amesema upatikanaji wa mhusika utalisainia jeshi hilo kujua sababu za jengo kuanguka.

Aidha, Majaliwa amesema serikali inakamilisha taratibu za uchunguzi kubaini chanzo cha ghorofa hilo kuanguka.

Advertisement

“Watakuwa na maswali ya msingi na yeye atashiriki kujibu maswali moja baada ya jingine,” amesema Majaliwa.