Majaliwa akagua ujenzi SGR Mwanza-Isaka

Majaliwa akagua ujenzi SGR Mwanza-Isaka

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo 26 Machi 2023 amekagua mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa SGR Mwanza-Isaka, kipande cha tano cha ujenzi wa reli awamu ya kwanza Dar es Salaam-Mwanza.

Kipande hiki cha Mwanza-Isaka kina jumla ya kilometa 341, hadi kukamilika kwake kitagharimu shilingi Trilioni 3.062. Kipande hicho kitakuwa na jumla ya vituo vya abiria 10 na vituo viwili vya mizigo vya Fela na Isaka.

Maendeleo ya ujenzi huo umefikia asilimia 28.03 na ujenzi wa tuta ni asilimia 58.4 sawa na kilometa 136 kati ya kilometa 249 za njia kuu.

Advertisement

 

Mradi huo umetoa ajira zaidi ya 6,720 na kandarasi ndogo zenye thamani ya shilingi bilioni 80 hadi sasa.

Baada ya kukagua mradi huo Waziri Mkuu Majaliwa amesema amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, huku akitoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa vifaa na mitambo inayotumika katika ujenzi huo.