Majaliwa apongeza mkakati nishati ya kupikia

DAR ES SALAAM; WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema mkakati wa nishati safi ambao umezinduliwa leo utakuwa chombo muhimu cha kuleta juhudi za pamoja na shirikishi kufanikisha ajenda ya utunzaji mazingira

Amesema hayo leo Mei 8, 2024 kwenye uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia wa mwaka 2024-2034, uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Amesema miongoni mwa vitu vilivyozingatiwa na kamati hiyo ya maandalizi ni pamoja na uwepo wa viongozi wa kisera, sheria, kanuni na miongozo iliyotolewa na Rais Samia na miongozo ya kitaifa na kimataifa inayohusika na nishati safi ya kupikia.

Amesema dira ya mkakati huo inamtaka kila Mtanzania kutumia nishati safi ya kupikia, ili kulinda afya, mazingira na kuboresha maisha.

Naye Naibu Waziri Mkuu na Nishati na Waziri wa Nishati Dk Dotto Biteko, amesema mkakati huo utahakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034

 

Habari Zifananazo

Back to top button