Majaliwa asisitiza uadilifu ujenzi mji wa serikali

Majaliwa apokea magari 51 uboreshaji uhifadhi wa utalii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali, wahakikishe wanazingatia uadilifu katika matumizi ya fedha, ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.

Pia amewaagiza Makatibu Wakuu wa Wizara zote, ambazo baadhi ya watumishi wake wake bado wako Dar es Salaam wahakikishe wanahamia Dodoma kama ilivyoelekezwa na Serikali. “ Simamieni agizo hili kikamilifu.”

Ametoa maagizo hayo leo Jumatatu, Septemba 5, 2022, wakati akizungumza baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua maendeleo ujenzi wa Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma, ambapo amewashukuru na kuwapongeza wakandarasi wanaojenga mji huo.

Advertisement

“Dhamira ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha ujenzi wa Makao Makuu unaendelea vizuri ni nzuri na lazima tujivunie maono ya viongozi na kazi nzuri wanayoifanya pamoja na kazi nzuri za wataalamu wetu,” amesema.

Amesema kuwa ujenzi wa mji wa Serikali utakuwa wa kisasa kwa kuwa utaendeshwa kidijitali: “Fedha za kutekeleza haya zipo na ninawahakikishia kila kitu kitakamilika, dhamira ya Rais Mheshimiwa Samia ni kufanya makao makuu kuwa bora zaidi.”

Amewasisitiza vijana wa Kitanzania wanaofanya kazi katika mradi huo waendelee kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uadilifu na waendelee kuzingatia maelekezo wanayopewa na viongozi wao, ili wawe na uwezo wa kujenga na kusimamia kazi zao.

Awali, Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Meshack Bandawe, alisema awamu ya pili ya ujenzi wa mji huo ilianza Oktoba 2022 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 2023. Mradi huo unahusisha majengo 25 ya wizara pamoja na majengo mawili ya taasisi za umma.

Bandawe alisema mradi huo ambao umefikia kati ya asilimia 39 na 45 unajengwa na wakandarasi tisa wakiwemo wa serikali na binafsi umetoa ajira 2,149.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *