Majaliwa aungana na Rais Samia kuomboleza kifo mbunge Mbarali

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameungana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa wananchi wa Jimbo la Mbarali na familia kwa ujumla kwa kufiwa na mbunge wa jimbo, Francis Mtega.

Taarifa za kifo cha Mtega zilitolewa jana jioni na Spika wa Bunge, Tulia Ackson.

Majaliwa amesema amepokea kwa mshtuko taarifa hizo, na kukiri kuwa katika kipindi cha uhai wake, Mtega alikuwa na mchango mkubwa katika Bunge na Wananchi wa Mbarali.

“Tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Amina.” Ameandika Waziri Mkuu, Majaliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button