Majaliwa kuzindua jengo la macho Bugando

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua jengo la macho katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Bugando , mkoani Mwanza.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu ujio wa Waziri Mkuu, anayetarajiwa kuwasili Jumamosi jioni kwa ziara ya siku nne.

‘’ Akiwa Mwanza atakagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Magufuli siku ya Jumapili na baadae atasalimia wananchi wa Busisi, kasha atawasili Usagara kusalimia wananchi,’’ amesema Malima na kuongeza kuwa kisha Waziri Mkuu ataenda Kwimba kukagua maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Dk Fabian Massaga, amesema jengo la macho litakalozinduliwa na Waziri Majaliwa limegharimu Sh bilioni 3.7

 

Habari Zifananazo

Back to top button