WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo Mei 17, 2023 kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mgomo wa wafanyabiashara hao.
Asubuhi ya leo wafanyabiashara hao waligoma kufungua maduka kwa madai ya utitiri wa kodi na tozo walizodai kutokuwa rafiki.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kuwa mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Anatouglou uliopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imesema kuwa kwa sasa serikali inaendelea kuwashawishi ili kuendelea na shughuli zao, wakati wanajipanga kuzungumza na wafanyabiashara hao.