DAR ES SALAAM: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Septemba 20, 2023 amefungua Kongamano la Tano na Maonesho ya Nishati Tanzania na amesema kwamba Serikali imedhamiria kuwa mzalishaji mkubwa na nishati.
“Tunaendelea na utafutaji wa gesi, tunataka tuwe wazalishaji wakubwa wa Nishati, tuwe na Umeme wa kutosha utakaopatikana kwa urahisi na nafuu na ziada tutauza nje ya nchi.“
Majaliwa ameyasema hayo baada ya kufungua kongamano hilo la siku mbili linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Amesema kuwa Tanzania haitegemei kuzalisha umeme kwa kutumia maji pekee bali inaendelea kuweka mkazo katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati nyingine kama gesi na jua.
Waziri Mkuu amesema katika kongamano hilo la kimataifa la nishati ambalo limehusisha viongozi na wadau kutoka katika mataifa mbalimbali Duniani litajadili namna bora ya kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa nishati.
Comments are closed.