Makalla: Rais Samia kuongoza zoezi la kupiga kura

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha mapinduzi(CCM) Taifa, Itikadi , Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza mamilion aya watanzania kwenda kupiga kura huku akusisitiza mfano mzuri kwa kushiriki kupiga kura akiwa Ikuru Chamwino.

CPA Makalla amesema hayo leo Novemba 26, 2024 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro ikiwa ni mwisho wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa ziliyofanyika katika mfululizo wa siku sita leo ikiwa ni ya saba na ya mwisho kwa ajili ya kupiga kura kesho Novemba 27, 2024.

Advertisement

Makalla amesema Rais Samia alianza kuonyesha mfano mzuri kwa kuanza na zoezi la kujiandikisha katika daftari la makazi ikiwa ni moja ya michakato ya mwanzo kuelekea kwenye uchaguzi huo.

“Rais wetu na mwenyekiti wetu atapiga kura kesho na sisi wote nchini na kwa mamlaka aliyopewa ametangaza kuwa kesho ni mapumziko ili wote tukapige kura,” amesema Makalla.

Aidha Makalla amewataka wananchi wafanye maombi kwa ajili ya Professa Jay kwa ajili ya kuimarika kiafya lakini wasimuombee apate vijiji huku akisisitiza kuwa CCM imepitia wakati mgumu jimbo lilivyoshikiliwa na wapinzani, hivyo aliwataka wajitahidi isijirudie.

“Tumuombe Profesa Jay apone lakini msimuombee apata kiji hata kimoja, ubinadamu tumefanya kila mtu kwa dini yake kumuombea afya njema lakini msiongeze maombi ya vijiji na mitaa,” amesema Makalla.