Makamba awasili Uholanzi ziara ya siku tatu

fursa za biashara Tanzania na Uholanzi zatajwa

THE HAGUE: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amewasili jijini The Hague, Uholanzi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia Novemba 13-15, 2023.
Katika ziara hiyo Makamba ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uholanzi litakalofanyika Novemba 14 na 15 Jijini The Hague.
Aidha, pembezoni mwa kongamano hilo, Waziri Makamba atapata nafasi ya kukutana na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Uholanzi, Kanke Bruins Slot. Kadhalika Makamba anatarajiwa pia kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi (Tanzania Diaspora).

online pharmacy periactin no prescription with best prices today in the USA

Waziri Makamba ameambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dk. Tausi Kida na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.

online pharmacy tobradex no prescription with best prices today in the USA

Daniel Mushi.

Wengine wanaoshiriki kwenye ujumbe wa Waziri ni Mabalozi na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali Serikalini yanayotafuta ubia na mashirika ya Uholanzi.

online pharmacy singulair no prescription with best prices today in the USA

Pia ujumbe wa Waziri Makamba umehusisha wafanyabiashara 16 kutoka sekta binafsi za Tanzania ambao watashiriki kwenye kongamano hilo.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button