Makamu wa Rais ataka ushirikiano kukuza Kiswahili

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah amewataka wahariri kushirikiana na mabaraza ya Kiswahili ya BAKITA na BAKIZA ili kuendeleza lugha ya Kiswahili.

Akizungumza leo, Julai 4,2023 mjini Zanzibar wakati wa mkutano na jukwaa la wahariri kuelekea Siku ya Kiswahili duniani amesema lugha ya Kiswahili imevuka mipaka na sasa kuna redio na runinga 38 duniani zinazorusha matangazo yao kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema lugha ya Kiswahili ipewe hadhi na ukubwa wake na mahali bora zaidi kuanzia ngazi ya jukwaa la wahariri ambao wanafanyakazi ya kutoa mwelekeo wa lugha na mambo mbalimbali kwa kusoma, kutazama na kusikiliza.

“Hamu yangu ni kukaa kwenye mkutano huu kuanzia mwanzo hadi mwisho bila kusikia neno la lugha nyingine zaidi ya lugha sanifu na sahihi ya Kiswahili” amesema Mwinjuma.

Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili ya mwaka 2023 ni ya pili baada ya kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2022 ambayo ni siku maalum ya kuadhimishwa lugha hiyo baada ya kutangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button