Makamu wa Rais Uganda avutiwa Makumbusho Dar

MAKAMU  wa Rais wa Uganda,  Jessica Alupo, ametembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam  na kuahidi kurudi tena, ili kujifunza  kwa kina  kuhusu masuala ya urithi adhimu wa historia ya Tanzania.

Alupo amepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dk Noel Lwoga na kupatiwa maelezo ya uhifadhi wa urithi wa utamaduni na historia kutoka kwa wataalam wa Makumbusho hiyo.

Amekuwa nchini  kuhudhuria mkutano wa wanawake na vijana katika biashara chini ya Mkataba wa Eneo huru la biashara Afrika, uliofunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.

Alupo ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa uhifadhi unaofanyika, kwamba ni eneo muhimu kwa ajili ya kupata historia mbalimbali pamoja na kujifunza jinsi watu wa kale walivyoweza kuishi.

“Nimefurahishwa sana na uhifadhi unaofanyika hapa, Makumbusho hii ipo vizuri maonesho na mpangilio wake uko vizuri, hongereni sana,” amesema  Alupo na kuongeza kuwa  makumbusho inasaidia jamii kutambua walipo na walikotoka..

 

Habari Zifananazo

Back to top button