Makonda mgeni rasmi Kitambi Noma Bonanza

ARUSHA: WAZIRI wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Bonanza la 10 la Kimataifa la Kitambi Noma litakalofanyika siku tatu na kuhitimishwa siku ya Pasaka.

Bonanza hilo litashirikisha timu 20 kutoka mikoa saba ambapo timu tatu kati ya hizo ni kutoka nchini Kenya na litachezwa kuanzia Aprili 3, 4 na kuhitimishwa Siku ya Sikukuu ya Pasaka Aprili 5.

Bonanza hilo limeandaliwa na klabu ya Kitambi Noma Veterani ya jijini Arusha likilenga kukutanisha wachezaji wa zamani kwa ajili ya kuimarisha na kukuza mahusiano kwa wachezaji .

Mwenyekiti wa Kitambi Noma Veterani, Robert Mbogoma amesema wanatarajia mgeni rasmi, kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Paul Makonda ambaye atatoa zawadi kwa washindi siku ya fainali yaani Aprili 5 mwaka huu.

Amesema kuelekea bonanza hilo kutatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Hisani Aprili 3,utakaozikutanisha timu ya Kijichi all stars ambao ndio mabingwa watetezi kutoka Dar es salaam watakaochuana vikali na Ndovu FC.

“Tunazisihi timu shiriki zisilete watoto kinyume na kanuni za mashindano na kusema sheria zitafuatwa kwa klabu itakayoleta wachezaji chini ya miaka 35 itaondolewa mara moja kushiriki,”amesema Mbogoma.

Amefafanua kuwa jumla ya viwanja vinne vitatumika ambavyo ni Future stars viwili, ISM na St Constantine ambapo kila kundi litajumuisha timu tano.

Timu shiriki zimepangwa Makundi manne yenye timu tano ambapo kundi A litahusisha Kitambi Noma-Arusha,Kivule Veteran-Dar es salaam, PBZ Veteran- Zanzibar, Mandingo veterani Tanga,Ndovus Fc -Nairobi.

Kundi B timu za Arusha All Star-Ars, Umoja Road veteran,Suka Veteran Dar es salaa,Kahawa veteterani ya Zanzibar na Chemba Veterani kutoka Dodoma.

Katika Kundi Kundi C timu za Kijichi All Star ya Dar es salaam, Rock City Veterani kutoka Mwanza,Uhuru Veterani-Moshi,Eagle Veterani-TangaEastlando Veterani ya Nairobi.

Kundi D Mwanza All star,Suka Orijinol kutoka Dar es saa., Alteza Travelling-Moshi, Burudani Vetrani Tanga na Mukuru Wazee-Nairobi.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….

    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I get paid more than $90 to $120 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.

    This is what I do….w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  3. The Secret to Work-Life Balance: I used to be stressed and overworked. Now, I’m earning over $220/hour working remotely, and I have more time for myself and my family. My friend’s success story inspired me to take the plunge. This incredible opportunity has allowed me to achieve the perfect work-life balance. I can now spend quality time with my loved ones, pursue my hobbies, and relax without worrying about money..

    Visit This…… w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button