Malawi kuondoa Jeshi lake Congo

MALAWI: RAIS wa Malawi, Lazarus Chakwera, amemuagiza Kamanda wa Jeshi la nchi hiyo kujiandaa kuondoa majeshi ya Malawi kutoka eneo la Mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Taarifa iliyotolewa na serikali imesema uamuzi wa Rais Chakwera unalenga kuheshimu tangazo la kusitishwa kwa mapigano kati ya pande zinazohasimiana, ingawa uamuzi huo wa kusitisha mapigano ulipangwa na waasi wa M23, ambao walifanya mashambulizi katika mji wa Nyabibwe katika Jimbo la Kivu Kusini, DRC.

Kuondolewa kwa wanajeshi wa Malawi kutatoa fursa ya kuendeleza mazungumzo ya kuelekea amani ya kudumu.Rais Chakwera amekumbana na shinikizo kubwa la kimataifa kuhusu uamuzi wa kuondoa majeshi ya Malawi Mashariki mwa DRC, hasa baada ya wanajeshi watatu wa Malawi kuuawa katika mashambulizi ya M23 mjini Goma.

Advertisement

SOMA: Malawi waondoa visa kwa nchi 79 duniani

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *