“Mama ni jasiri na sina mashaka naye”- Bagonza

KAGERA: ASKOFU wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk.Benson Bagonza amesema maamuzi ya kusaka maridhiano katika makundi mbali mbali ikiwemo vyama vya siasa yaliyofanywa na Rais, Samia Suluhu Hassan ni ya ujasiri na yenye gharama za kisiasa.

Dk.Bagonza amesema hayo wilayani Karagwe katika sherehe za kuweka Wakfu Kanisa Kuu Lukajange lilipo wilayani hapa ambapo amesema Kanisa ni alama ya upatanisho.

Advertisement

“Kanisa ni moja ya alama ya upatanisho na moja ya R ya Rais wetu, Dk.

Samia inamaanisha Reconciliation, yaani upatanisho.Napenda kumpongeza Rais wetu kwa ujasiri wenye gharama za kisiasa pale alipodiriki kuingia katika mchakato huo wa maridhiano.

“Mama ni jasiri na sina mashaka naye. Upatanisho mahali popote una baraka za Mungu , na anayesita au kuvuruga upatanisho anafarakana na Mungu, napenda kumshukuru Rais kwanza kwa kuniamini na kunishirikisha katika jitihada hizo za maridhiano.” Amesema Askofu Bagonza na kuongeza

“Kupitia Hekalu hili napenda kumtia moyo , na naomba mumpelekee ujumbe wangu asiache kushughulikia maridhiano katika taifa letu kwa sababu kuridhiana ndio afya ya taifa letu, na katika maridhiano aliangalia makundi mbalimbali.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuzungumzia tatizo la ajira nchini ambapo amesema pamoja na jitihada kubwa za Serikali katika eneo hili kuna mambo mawili lazima kuyakubali hata kama yanaumiza na yanagharama kisiasa.

pharmacy

“La kwanza Serikali haina uwezo wa kuajiri wahitimu wote nchini , Serikali yenye uwezo huo haipo duniani kokote ambako nimewahi kutembea , najua linauma lakini lazima tukubali ukweli.Pili elimu yetu inaanda watu kuajiriwa badaa ya kujiajiri kwa hiyo tusiwabeze wanaotafuta kazi maana ndicho waliochoendea shule.

“Walienda shule ili watafute kazi, hivyo tusiwabeze, sasa kutokana na ukweli huu mchungu napenda kuishauri Serikali mambo mawili, ” amesema.

Amesema kwanza serikali itengeneze sera rafiki, kuiwezesha sekta binafsi, muwekezaji na wadau wengine wa maendeleo ili kila muajiri apate nafuu ya namna fulani kumuwezesha kuajiri watu wengine zaidi.

Alitoa mfano kila mwajiri anayeajiri watu zaidi ya 10, Serikali imsaidie kulipa asilimia 10 iende NSSF, kwa masharti kuwa alipe mshahara usio chini ya kima cha chini cha mshahara kilichokubaliwa kisheria.

Ameongeza vivutio vya namna hiyo kama msamaha wa kodi, au tozo kadhaa pamoja na nafuu zingine za waajiri zinaweza kumeza sehemu kubwa ya vijana wasio na ajira.

1 comments

Comments are closed.