Mambo manne yatajwa kupaisha uchumi

DODOMA – PATO halisi la Taifa limefi kia Sh bilioni 148,399.76 mwaka 2023 kutoka Sh bilioni 141,247.19 mwaka 2022, sawa na ukuaji wa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 4.7 mwaka 2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo aliliambia Bunge mjini Dodoma jana wakati akielezea Mwelekeo wa Hali ya Uchumi kwa mwaka 2024/2025.

Alisema ukuaji huo wa uchumi ulichangiwa na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ikiwemo mikakati ya kukabiliana na athari za vita kati ya Ukraine na Urusi na uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu na usafirishaji.

Mambo mengine yaliyochangia ni kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususani dhahabu na makaa ya mawe na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi iliyochachua shughuli za kiuchumi.

SOMA: Tril 15.94/- kugharimia shughuli za maendeleo

“Hata hivyo, kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa cha asilimia 5.1 mwaka 2023 kipo chini ya lengo la mwaka la asilimia 5.2, hii ilitokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji katika baadhi ya sekta,” alisema.

Alisema pia mabadiliko ya tabianchi yaliathiri uzalishaji katika sekta ya kilimo kwa baadhi ya maeneo nchini na kuharibu miundombinu ikiwamo madaraja na barabara pamoja na hatua zilizochukuliwa na nchi zilizoendelea katika kukabiliana na mfumuko wa bei zilizosababisha kuongezeka kwa gharama za mikopo kutoka masoko ya kimataifa ya fedha na hivyo kuathiri shughuli za uzalishaji.

Kuhusu mwenendo wa ukuaji wa uchumi na mchango wa ukuaji katika kila robo ya mwaka kuanzia mwaka 2019- 2023, Kitila alisema mwaka 2023, sekta ya sanaa na burudani iliongoza kwa kuwa na ukuaji wa asilimia 17.7

Habari Zifananazo

Back to top button