Mambo mazuri yanukia uchimbaji madini ya Kinywe

WAZIRI wa Madini Dk Dotto Biteko, amewataka wananchi wa Kijiji cha Namangale katika Halmashauri ya Mji wa Mtama, mkoani Lindi kutoa ushirikiano kwa mwekezaji wa Madini ya Kinywe Volt Resources Limited, ili aweze kulipa fidia kwenye maeneo yatakayojengwa mgodi.

Dkt. Biteko alisema hayo jana Juni 18, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Namangale, mkoani Lindi ambapo amesema mgodi huo utasaidia kuongeza ajira na kuchochea maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho kupitia shughuli za uchimbaji madini.

Pamoja na mambo mengine, Dk Biteko amesema Kampuni ya Volt Resources Limited kutoka nchini Australia itakayochimba madini hayo inatarajiwa kuwekeza zaidi ya Dola za Marekani milioni 40 katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa mgodi huo,  ambapo inakadiriwa kuwa na hifadhi ya zaidi ya tani milioni 461 za madini ya Kinywe katika kijiji cha Namangale Mkoani Lindi.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, ameiomba Wizara ya Madini kuisimamia kwa karibu Kampuni ya Volt Resources Limited ili kuhakikisha mradi wa uchimbaji wa madini ya  Kinywe katika kijiji cha Namangale unaharakishwa, ili wananchi wa Mkoa wa Lindi wapate ajira.

Pamoja na mambo mengine, Nauye amesema Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameufungua Mkoa wa Lindi, ambapo kwa sasa Taifa linashuhudia miradi mingi ya maendeleo ikifanyika mkoani humo, ukiwemo mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe unaotarajiwa kujengwa katika kijiji cha Namangale.

Katika ziara hiyo Dkt. Biteko ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unaanza kulipa fidia wananchi, ili uanze uzalishaji kwa wakati.

Kinywe katika kijiji cha Namangale unaharakishwa ili wananchi wa Mkoa wa Lindi wapate ajira.

Pamoja na mambo mengine, Nauye amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameufungua mkoa wa Lindi ambapo kwa sasa Taifa linashuhudia miradi mingi ya maendeleo ikifanyika mkoani humo ukiwemo mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe unaotarajiwa kujengwa katika kijiji cha Namangale.

Katika ziara hiyo Dkt. Biteko ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unaanza kulipa fidia wananchi ili uanze uzalishaji kwa wakati.

Habari Zifananazo

Back to top button