Mambo yakuzingatia unaponunua TV mpya

DAR ES SALAAM: Jina “Mini LED” kwenye boksi la televisheni linaweza kumvutia mnunuzi anayetarajia kupata picha yenye ubora wa juu, lakini wataalamu wanaonya kuwa jina hilo pekee halitoshi kutathmini uwezo wa televisheni.

Tofauti ya ubora kati ya televisheni zinazotumia teknolojia hiyo inaweza kuchangiwa na namna taa ndogo zinazotumika kuangaza paneli zilivyopangwa na jinsi mwanga unavyodhibitiwa.

Mini LED hutumia taa ndogo sana nyuma ya paneli, hali inayowezesha kuwekwa kwa taa nyingi zaidi na kugawanywa katika maeneo yanayoweza kudhibitiwa kwa kujitegemea.

Mfumo huo unapotekelezwa vizuri, husaidia kufanya maeneo meusi ya picha yaonekane meusi zaidi, huku sehemu zenye mwanga zikibaki angavu na zenye undani.

Kwa mujibu wa maelezo ya TCL, mojawapo ya mambo muhimu kwa mnunuzi ni kuangalia kama televisheni ina hardware local dimming, mfumo unaowezesha kupunguza au kuongeza mwanga katika maeneo tofauti ya skrini.

Mfumo huo unatofautiana na kutegemea programu pekee katika kuchakata picha, kwa kuwa local dimming huwezesha udhibiti wa mwanga katika maeneo maalumu nyuma ya paneli.

Jambo la pili ni idadi ya dimming zones, ambazo ni maeneo ya mwanga yanayoweza kudhibitiwa kwa kujitegemea.

Kwa mazingira yanayofanana, idadi kubwa ya maeneo hayo inaweza kusaidia kutoa udhibiti wa mwanga ulio sahihi zaidi. Hata hivyo, idadi ya maeneo pekee haipaswi kuwa kipimo cha mwisho, kwa kuwa namna mfumo mzima unavyofanya kazi pia huathiri ubora wa picha.

Jambo la tatu ni namna taa hizo zilivyopangwa nyuma ya paneli.

Mfumo wa Full Array Local Dimming (FALD) husambaza taa nyuma ya paneli na kuruhusu mwanga kudhibitiwa katika maeneo mbalimbali ya skrini.

Kwa TCL, FALD ni sehemu muhimu ya mfumo unaotumika katika televisheni zake za Mini LED, huku kampuni hiyo ikiwahimiza wanunuzi kuangalia zaidi ya jina la teknolojia wanapolinganisha bidhaa za chapa mbalimbali.

Kwa hiyo, kabla ya kununua televisheni yenye alama ya Mini LED, mnunuzi anashauriwa kuuliza kuhusu mfumo wa local dimming, idadi ya dimming zones na mpangilio wa taa nyuma ya paneli.

Hatua hiyo inaweza kusaidia kufanya uamuzi kwa kuzingatia teknolojia inayotengeneza picha, badala ya kutegemea jina la teknolojia lililoandikwa kwenye boksi pekee.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button