Mambo yazidi kunoga Bwawa la Nyerere

WAZIRI wa Nishati January Makamba amesema wameridhishwa na kasi ya ujazaji maji Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power.

Amesema kwa sasa ujazo wa maji umefika mita za ujazo bilioni 6 na kwamba zimebaki chache tu, kufikia kiwango cha maji yatakayoweza kuzungusha mitambo ya kufua Umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa kiwango hiko ni kizuri na kimezidi matarajio yaliyokuwepo awali wakati wa uzinduzi wa ujazaji maji uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Maendeleo mazuri ingawa kazi bado ipo. Kwa mujibu wa takwimu, kiwango cha maji yaliongia wiki mbili zilizopita, ni mengi kuliko maji yaliyoleta mafuriko 2019/2020.

“Hii maana yake kwa neema ya mvua iliyopo kwa sasa, zile athari za mafuriko zilizokuwepo siku za nyuma hazipo tena. Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko.

“Kwa sasa ujenzi wa bwawa kwa ujumla uko asimilia 86. Wakati Mheshimiwa Rais Samia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37,”  amesema Waziri Makamba.

Habari Zifananazo

Back to top button