Mamia wajitokeza msaada wa kisheria Missenyi

MAMIA ya wananchi wanaoishi Kata ya Nsunga vijijini vya Byamtemba, Igayaza na Ngando wilayani Missenyi wamejitokeza kwa wingi kuwasilisha kero kwa wataalamu wa kisheria ambao wamekuja kusikiliza na kutatua changamotoo za kisheria kupitia kampeini ya huduma za kisheria ya Mama Samia

Hii ni siku ya kwanza kwa wilaya hiyo mara baada ya uzinduzi wa kampeini ya msaada wa kisheria iliyozinduliwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dk Damas Ndumbaro mkoani Kagera ambayo itatekelezwa kuanzia Aprili 14 – 23 mwaka huu.

Advertisement

Mamia ya wananchi waliojitokea katika viwanja vya Igayaza kata ya Nsunga wakiwa na shauku ya kuwasilisha changamoto zao na wengi wanasema hii ni mara ya kwanza kushuhudia wananchi wakaifuatwa na timu ya mawakili na wanasheria kwenda kuwasililiza na kuwapa elimu ya kisheria tangu nchi ya Tanzania imepata uhuru.

“Kama wananchi tumefurahishwa na tukio la mama Samia kuleta huduma za kisheria wengi hawana uzoefu hata wakitapeliwa wanajiuliza tutaenda kwa nani ,tutaanzia wapi ,uwepo wa huduma za kisheria katika vijiji vyetu ni mwanga tosha kuwa serikali inawajali wananchi wake ,Hili ni jambo kuwa na ni faraja kwa wananchi wa wilaya ya Missenyi na Tanzania kwa ujumla,” amesema Reondar Lucas kutoka kijiji cha Igayaza

Mratibu wa kampeini hiyo Wilaya ya Missenyi Maximilian Fransis amesema kuwa zaidi ya wananchi 1,000 wamejitokeza kupata elimu ya kisheria katika viwanja vya Igayaza na walifika kabla ya saa 3 asubuhi.

Amesema lengo la wataalamu waliokija kutekeleza kampein hiyo ni kuhakikisha wanatoa elimu ya uhakika kwa wananchi wa wilaya hiyo ili kuwasaidia kuokoa muda mwingi ambao wanatumia mahakamani badala ya kufanya shughuli za kuzalishaji

Amesema kuwa malengo ni kutatua migogoro yote ya kisheria asilimia 75 kwa vijiji 30 vya wilaya ya Missenyi ambavyo vitatembelewa hivyo wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kwani gharama za Kuwahudumua kisheria zimelipwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *