Mamilioni ya watu kukosa umeme

CUBA : SHIRIKA la umeme nchini CUBA limesema linauwezo mdogo wa kusambaza umeme megawati 533 tu kati ya megawati zaidi ya 3,000 zinazohitajika.
Mapema serikali ya nchini humo imesema kipaumbele kwa sasa ni kupeleka umeme mahospitalini na vituo vya kusambaza maji na mashuleni na huduma zisizo za lazima za serikali zimefungwa hadi hapo baadaye.
Mji mkuu wa Havana unaendelea kusalia kwenye giza ingawa Shirika hilo la umeme kudai imetoa huduma hiyo kwa zaidi ya wateja 260,000 waliohitaji huduma ya umeme.
Utoaji wa huduma ya umeme nchini Cuba unadaiwa kushindwa kutokana na uhaba wa mafuta, majanga na mizozo ya kiuchumi. SOMA : Rais Mwinyi awasili Cuba



