TETESI za usajili zinasema Manchester United imerejea katika mazugumzo na Barcelona kuhusu kumsajili Frenkie de Jong.
Miamba ya Catalan inahitaji kumuuza mchezaji wa kiwango cha juu majira haya ya kiangazi kuimarisha uwezo wao wa kifedha. (El Nacional – Spain)
SOMA: Barcelona yagoma kuuza 7 majira ya joto
Mshambuliaji Victor Osimhen anapenda kujiunga na Chelsea badala ya PSG iwapo ataruhusiwa kutimiza matarajio yake ya kuondoka Napoli majira haya ya kiangazi. (CalcioNapoli24)
Barcelona imewasilisha ombi jipya la kumsajili Dani Olmo ambalo linalingana na uthamini wa RB Leipzig wa Euro milioni 60 wa nyota huyo wa kihispania. (SPORT – Spain)
Arsenal iko nyumba ya mpinzani wake Tottenham Hotspur katika mbio za kumsajili winga wa Wolves Pedro Neto, huku Spurs ikizidisha mazungumzo na kambi ya kireno kuhusu vipengele binafsi. (Football Transfers)