Manula atimkia Sauzi kwa matibabu

Aishi Manula

KIPA wa Simba SC, Aishi Manula amepelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na majeraha.

Manula amekuwa nje ya dimba tangu mwanzoni mwa mwezi April na hivyo kuikosa baadhi ya michezo muhimu ya timu hiyo.

Taarifa iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii ya Simba imeeeleza kuwa Manula tayari amewasili nchini humo ili kupata matibabu ya majeraha yanayomsumbua.

Advertisement

1 comments

Comments are closed.