Maonesho Sabasaba yaendelea kutoa elimu

MAONESHO ya 47 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya SabaSaba yanaendelea kutoa fursa kwa wadau mbalimbali kujifunza namna kampuni mbalimbali zinavyoweza kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali.

Hatua hiyo ni baada ya wadau mbalimbali kushuhudia kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) inavyotekeleza Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Advertisement

Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk Venance Mwasse Julai 4, 2023 alitembelea banda la GGML katika maonesho hayo na kujifunza masuala mbalimbali.

Dk Mwasse alipata maelezo kutoka kwa ofisa manunuzi (mikataba) wa GGML, Silas Shija (wa kwanza kulia) aliyekuwa ameambatana na Scholastica Hoya, ofisa Rasilimali watu na Innocent Mushi ambaye ni ofisa Mwandamizi (Rasilimali Watu).

Maofisa hao walieleza jinsi GGML inavyosaidia miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika jamii zinazozunguka migodi yake kama vile elimu, afya, maji, miundombinu na kilimo.

Miradi hii inaakisi dhamira ya GGML kwa jamii inayozunguka mgodi kuwa na maendeleo endelevu ambapo moja ya maadili yake ya msingi na maono yake ni kutoa mchango chanya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *