Mapigano mashariki ya kati yasitishwe -UN

MAREKANI : AFISA wa Umoja wa Mataifa Tor Wennesland amesisitiza umuhimu wa kusitisha kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na kuitisha mazungumzo ya amani kati ya nchi hizo mbili kwa lengo la kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.

Wennesland  amesema  mapigano yanayoendelea katika ukanda huo ni hatari zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali jambo ambalo linahitaji kutafutiwa suluhisho la kudumu.

Akizungumza  katika kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Mashariki ya Kati na suala la Wapalestina, ,Wennesland amesema ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa haitawezekana kuibadili hali inayoendelea sasa katika Ukanda wa Gaza.

Advertisement

Kwa upande wake,muangalizi wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour amesema vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza vimewafanya Wapalestina wengi kukata tamaa ya maisha  huku wengine wakihofia maisha yao.

Mansour  ameendelea kuikosoa Israel kwa kutoheshimu sheria za kimataifa kwa kuvunja baadhi ya sheria za Umoja wa Mataifa.

SOMA : Euro milioni 50 kusaidia Gaza