Euro milioni 50 kusaidia Gaza
BERLIN : WAZIRI wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Berlin itaongeza misaada ya kibinadamu yenye thamani ya Euro milioni 50 kuwasaidia wananchi wa ukanda wa Gaza.
Akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa Jordan, Ayman al- Safadi mjini Amman,Baerbock amesema kiasi kilichotolewa na Ujerumani kwa Ukanda wa Gaza tangu mwaka jana ni zaidi ya Euro milioni 360.
Misaada hiyo itaelekezwa katika kupambana na njaa, utapiamlo pamoja na utoaji wa huduma za afya.
SOMA : Blinken na Hakan waamua kusitisha mapigano Gaza
Ujerumani pia itaongeza msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wa Syria walioko Jordan kwa Euro milioni 12.7, na kuongeza msaada huo hadi kufikia Euro milioni 63.